Exodus 26:15-20

15“Tengeneza mihimili ya kusimamisha ya mti wa mshita kwa ajili ya maskani. 16Kila mhimili uwe na urefu wa dhiraa kumi
Dhiraa 10 ni sawa na mita 4.5.
na upana wa dhiraa moja na nusu,
17zikiwa na ndimi mbili zilizo sambamba kila mmoja na mwingine. Tengeneza mihimili yote ya maskani jinsi hii. 18Tengeneza mihimili ishirini kwa ajili ya upande wa kusini wa maskani, 19 bkisha tengeneza vitako arobaini vya fedha vya kuweka chini ya hiyo mihimili, vitako viwili kwa kila mhimili, kimoja chini ya kila ulimi. 20Kuhusu upande wa kaskazini wa maskani, tengeneza mihimili ishirini
Copyright information for SwhKC